Siri 1 Kuu Ya Kudeti Na Kutongoza Ambayo Wanaume Wengi Hawaijui


Kama umekuwa ukijiuliza ni wakati gani ambapo hisia za kupendana zinakuja kwako na kwa mwanamke acha nikuambie ukweli...si mara ya kwanza ambapo mtakutana kwa deti bali ni mara ya pili. Hapa ndipo uhusiano kati yenu wawili wa kimapenzi unaanza.

Hili ndilo tatizo kubwa ambalo wanaume wengi wanakosa kulielewa. Unapata mwanaume anarusha silaha zake zote siku yake ya kwanza ya deti na mwanamke...kosa kubwa kabisa.

girls, date, women, love

Ok najua sahizi unafikiria nini. Ya nini kukutana na mwanamke deti ya pili ilhali unaweza kufunga bao mara ya kwanza mnapokutana? Well, sikatai ya kuwa si vibaya kufunga mchezo siku ya kwanza. Mwanzo mimi ni miongoni mwa wale ambao wanajivunia kupata mgao wa nafasi kama hio.

Lakini niamini nikikuambia ya kuwa baada ya muda flani itafikia level ambayo utaacha gemu yako ya kuapproach wanawake na utataka kutafuta mwanamke wa kawaida ili uanze mahusiano ya level nyingine. Kufanya mapenzi ni mwanzo tu. Hivyo ni bora uanze kutafuta mwanamke ambaye analingana na wewe kimawazo na mtizamo. [Soma: Tongoza kama bingwa kwa kufuata hatua hizi]

KILE NTAKACHOKUAMBIA SAHIZI KITAKUSHTUSHA...

Mawaidha mazuri ambayo nataka nikuambie ni kuwa jiepushe na kufanya mapenzi siku ya kwanza ambapo utadeti ama kumtoa out mwanamke. Jikontrol na ujizuie usionyeshe hisia zako za mapenzi hadi wakati mwingine ambapo mtameet. Sababu ya kusema hivi ni rahisi. Mtakuwa mmebadilisha akili yenu kutoka kudeti kikawaida hadi kudeti kunakoonekana serious. Hii itakuwa deti ya hakika ambapo pia yeye atachukulia vivyo hivyo.

Sababu nyingine ambayo hufai kufanya mapenzi deti yenu ya kwanza ni 'kujutia baada ya kucha'. Hii mara nyingi hutokea kwa wanawake ambapo wanajutia kwa kitendo walichofanya usiku uliotangulia. Hapa wanawake wanaweza kuingiwa na hisia za kujutia za kuwa walishindwa kujizuia kufanya mapenzi wakati ambapo walikuwa katika deti...mara nyingine hii inaweza kumwathiri mwanamke kiasi cha kuwa anaweza kushindwa kuendelea na mahusiano yenu. [Soma: Jinsi ya kujizuia kufanya mapenzi]

Ok. Je namaanisha ya kuwa deti yako ya kwanza na mwanamke unayempenda hufai kulenga nyota yako kwa kutumia ujuzi wako wote wa kumteka hisia? La hasha.

Lile ambalo nasistiza ya kuwa mambo mengine unafaa kuyahifadhi hadi deti yako ya pili. Kufanya hivi kutamfanya mwanamke kujiskia huru kuongea zaidi kujihusu huku akijiamini ya kuwa bado ana uwezo wa kutumia ujanja wake kama mwanamke.

Kufanya mapenzi na mwanamke kunamfanya kujihisi kama yuko uchi. Pia atakuwa akiingiwa na maswali ya iwapo kama unampenda kweli ama uko hapo kumtumia kujiridhisha wewe mwenyewe binafsi.
Ajenda yako kuu ni kutaka kumfanya mwanamke kama huyu akuone kama boyfriend wa maisha yake. Ama sivyo? Hii inamaana ya kuwa mapenzi utakuwa ukifanya naye muda wote ukijumlisha ya kuwa na mahusiano marefu kati yenu.

So siri ya kufanikiwa hivi ni nini? Rahisi. Ni kumfanya ajiskie huru, kujenga kizingiti cha uhusiano wenu na kumfanya ajitolee kukujua zaidi....hivi vitu vitatu vitajenga mahusiano ya nguvu siku ya pili mtakapokutana katika deti. [Soma: Hatua za kumzuzua mwanamke akupende milele]No comments:

Jiunge na jamii yetu ya Facebook/App yetu ili uweze kutangamana na members na readers wetu wa Nesi Mapenzi ama ujitafutie mpenzi HAPA

Powered by Blogger.