Njia 9 Unazohitaji Kutumia Kumtongoza Mwanamke Ambaye Hamko Ligi Moja Naye

Jinsi ya kutongoza na mapenzi
Ni mwanamke ambaye akiingia mahali kila kitu kinasimama na kumuangalia yeye. Kila akipita watu wanamkodolea macho ya kuingiwa na tamaa. Kila anapotembea unajiskia dunia yote ikikuzunguka kichwani. Kiufupi ni mwanamke mrembo unayemzimia kiasi cha kuwa unashindwa kumtongoza. [Soma: Mapenzi na sababu 9 za kwa nini watu hupenda]

Kama wanaume wengine, unashindwa kumtongoza kwa sababu anaoneka level nyingine, yaani ni tofauti kabisa na mwanamke wa kawaida. So utafanya nini ili kumpata mwanamke kama huyu?

Usikate tamaa kwani kama mwanaume yeyote, pia wewe una nafasi bora ya kumnyakua mwanamke huyo na kumfanya wako kabisa. Ujanja ni kufuata haya maagizo ambayo yamefanyiwa utafiti na kudhibitishwa kuwa yanafanya kazi asilimia mia moja.

Zifuatazo ni jinsi ya kutongoza mwanamke aina hii:

1. Kuwa na sababa za uhakika
Kabla kuanza chochote, unafaa kujiuliza kwa nini unataka kumtongoza huyo mwanamke. Najua hautaki kumtongoza kwa sababu ya umbo lake ama unataka kujionyesha kuwa wewe ni bingwa kutongoza mademu warembo zaidi manake ukifanya hivyo utakuwa umejidhalilisha kimpango flani. Pia usijaribu kumtongoza ili kumuonyesha mpenzi wako wa zamani kuwa hatoshi mboga. [Soma: Jinsi ya kumuiba mwanamke ambaye ana boyfriend]
Pili unafaa kuifahamu miondoko ya msichana mwenyewe kiufupi, yaani kuyajua maisha yake, vitu anavyovipenda, na pia je mkiwa pamoja mnaweza kuunganika. Ukihakikisha kuwa sababu zote unazo za kumtongoza mwanamke huyu, basi sasa unafaa kuruka kwa step ya pili.

2. Kuwa gentleman
Kujifanya sharobaro kwa mwanamke aina hii huwezi kutoboa hata mara moja. So nilazima utumie maujanja ya kuwa mnyenyekevu kwa kila mmoja. Usiwe mtu ambaye unaropokwa na kutusiana na wanawake ovyo ovyo. Unafaa ujaribu kadri uwezavyo kuheshimu kila mtu. Hii ataona kuwa wewe unadalili za kuwa mwanaume bora zaidi wa kuwa naye.[Soma: Vitu ambavyo mwanamke angependa kutoka kwa mwanaume]

3. Kuwa mcheshi
Wanawake hupenda wanaume wacheshi, yaani mtu ambaye anaweza kumfurahisha na kujiskia na furaha wakati wote. Ok kuna wanaume ambao ni vigumu wao kumchekesha mwanamke lakini hio si sababu ya kuwa hautakuwa na nafasi ya kumpata mwanamke wa ndoto zako. Hakikisha hata kama ni mara moja unahifadhi baadhi ya vitu ambavyo kwa hakika vitachekesha. Na amini usiamini, wakati ambapo utakuwa ukimfurahisha, itakuwa rahisi kwako kuwa na nafasi rahisi ya kuuteka moyo wake.[Soma: Jinsi ya kumchekesha mwanamke]

4. Kuwa karibu naye
Hapa simaanishi kuwa kila mahali atakapokuwa unamfuata nyuma nyuma kama fisi, la. Kile ambacho namaanisha hapa ni kuwa uhakikishe kuwa atleast una company na yeye. Hii inaweza kufanikishwa kiurahisi kama wewe ni rafiki wa rafiki yake. Unaweza kuitisha kikao na rafiki yako halafu umwambie amkaribishe rafiki yake (huyo mnayemzimia). Hapo itakuwa rahisi kwako kueneza mbinu ya 3 hapo juu kwa urahisi.
Onyo: Usianze kumtongoza papo kwa papo...anza na kumfanya akuzoee halafu mengine yatakuja baadae.[Soma: Mfanye mwanamke apagawe aanze kuvutiwa kwako]

5. Kujiamini
Kujiamini ni lazima. Bila kujiamini mwanamke kama huyo hutampata. Hii ni kwa sababu aina kama hii ya mwanamke kwa mara nyingi huwa na maringo ambayo wakati mwingine wanaume wengi wanaona kama ni madharau. Hii ndio mbinu kuu ya mwanamke kama huyu hutumia ili kuhakikisha amejitenga na baadhi ya wanaume. So wewe kama wewe mwanamke kama huyu unafaa kumchukulia kama binadamu wa kawaida. Ukishafanya hivyo, itakuwa rahisi kwako kwani utakuwa umejitenga na kategoria ya wanaume waoga kwa mbali. [Soma: Jinsi ya kumtongoza mwanamke kwa njia ya kirafiki]

6. Muonyeshe uzuri wako
Hapa lazima umuonyeshe talanta yako yeyote ambayo unayo. Aidha unaweza unakipawa cha kuimba, kuchora, kudensi, kubendua maungo nk. Owk utajiuliza kwa nini unafaa umuonyeshe talanta yako. Jibu ni rahisi. Wewe hautakuwa pekeako kumtamani ama kumtongoza, so lazima uje na kitu ambacho kitakutofautisha na wanaume wengine ili asikusahau. Ukimwonyesha kipawa chako labda anaweza kukukubali na akapenda mambo yako na kumfanya kutamani kuwa na wewe mara kwa mara.

7. Tafuta udhaifu wake
Kila mwanamke anaudhaifu wake katika vitu na mambo tofauti tofauti. Hakikisha umejua udhaifu wake vizuri. Kama anampenda mwanamziki flani, sehemu fulani ama chochote kile, hakikisha umejipatia nafasi ya utafiti ili wakati mwingine utakapokutana na yeye unazua stori kuhusu jambo analolipenda. Atachangia na wewe ujazie. Hii itakufanya wewe kuweza kukupenda kwani ataona kuwa kuna mfanano kati yenu kwa vitu mnavyopenda. [Soma: Maswali mazuri ya kutongoza kumuuliza mwanamke]

8. Makinika na akili yake na wala si umbo lake
Kama tulivyotangulia kusema, ni kuwa wanawake ambao hamko ligi moja nao kwa kawaida wanajitambua kuwa wao ni warembo kupindukia. So wataona kama wanachoshwa kuambiwa kuwa ni warembo, so kile ambacho unachohitaji kushungulikia zaidi kumsifu kwa mambo ambayo anayoyafanya na kupitia akilini mwake. Baada ya kuongea na yeye katika maongezi tofauti tofauti, atakufungulia moyo wake kwa urahisi ambapo hapo utatumia nafasi kumjua kiundani kumhusu. Akitaja kitu ambacho kimekupendeza unaweza kutumia nafasi hio ya kumsifu na kumwambia kuwa umependezwa sana kwa kutaja au kugusia swala fulani.

9. Jaribu kuja na kitu tofauti

Kama imetimia ule muda wako ambao unaona kuwa umefikia level ya kumfungilia moyo wako na kumwambia kuwa unampenda, jaribu kufanya kitu tofauti ambacho hajawahi kufanyiwa na yeyote. Usijaribu kumpelekea maua kwani hio inaweza kuwa si mara yake ya kwanza kupokea maua so kama ni wewe ungefanya uchunguzi na kitu ambacho bado unaona hajawahi kuletewa so ukifanikiwa kumsaprize vizuri, una nafasi kuu ya wewe kufanikiwa kumpata yule aliyendotoni. [Soma: Jinsi ya kutongoza kama bingwa kwa wanaoanza]

Haimaanishi kuwa mwanamke ambaye hayuko ligi yako huwezi kufanikiwa kumtongoza. Ukitumia ujanja ambao ni tofauti na wanaume wengine una nafasi kubwa ya kufaulu. Kutumia ujanja wako vizuri na kujiamini ni kama mkuki kwa mwanamke, ukiurusha haukosi kutoboa.
Njia 9 Unazohitaji Kutumia Kumtongoza Mwanamke Ambaye Hamko Ligi Moja Naye Njia 9 Unazohitaji Kutumia Kumtongoza Mwanamke Ambaye Hamko Ligi Moja Naye Reviewed by Admin on 10:36 AM Rating: 5

5 comments:

 1. Hapa umeongea vizuri. Kuna dem ninayemfukuzia lakini amekuwa na maringo hataki kuitikia. Ngoja nifuate hizi mbinu halafu nikirudi naja kukuambia mbila kitu

  ReplyDelete
 2. So true asee, this might work, lem go for it, thank you 👏

  ReplyDelete
 3. utatumia njiagani kumpata binti wa kilokole iwapo wewe ni kanisa tofauti.mfano rc,sabato n.k

  ReplyDelete
 4. naomb unisaidie mimi nina aibu sana nashindwa kumtongoza.nifanyaje?

  ReplyDelete

Jiunge na jamii yetu ya Facebook/App yetu ili uweze kutangamana na members na readers wetu wa Nesi Mapenzi ama ujitafutie mpenzi HAPA

Powered by Blogger.