Jinsi Ya Kumvutia Mwanamke Ambaye Tayari Ana Mchumba


Kuna aina flani ya wanaume ambao hupenda sana kutongoza wanawake ambao wana wachumba tayari. Utapata siku zote alikuwa anamuona huyu mwanamke akiwa singo lakini hakuna hata siku moja alichukua hatua ya kumuaproach. Lakini ile siku ameskia amepata boyfriend ndio unaona jamaa huyu anajitikeza unyo unyo anamnyemelea mwanamke huyu.

Jinsi Ya Kumvutia Mwanamke Ambaye Tayari Ana Mchumba

Well, sijakataa. Kila mtu anakuwa na tabia zake na sababu zake. Wengine labda wataamua kutongoza mwanamke ambaye ana mchumba kwa kuwa labda analipiza kisasi, labda ana wivu ama sababu yoyote ile.

Uzuri ni kuwa usaidizi upo. Kuna mambo ambayo ukifuata mwanamke kama huyu utamtongoza na akubaliane na wewe haraka. Zama nasi.

#1 Kuwa mwanaume ambaye anakuwa kwa ndoto ya kila mwanamke.
Kuwa na tabia za kigentleman. Ukiwa na tabia za gentleman itamfanya mwanamke yeyote yule akuwaze na kukutia ndotoni mwake na pia kutaka kukujua zaidi ama atleast kuwa na uwezekano wa yeye na wewe kukutana mara kwa mara.

Pia kando na kuwa na tabia za ugentleman, hakikisha ya kuwa unapenda kuwa karibu na yeye. Akianza kuonyesha dalili zozote zile, mfano kukupa busu kipajini au kwa shavu, ama kupenda kukukumbatia, fahamu kuwa unaenda sambamba na ajenda yako. Pia kumfanya akuweke kwa akili yake lazima uonyeshe interest zako kwake. [Soma: Hatua za kufuata kupata girlfriend wa kwako]

#2 Usiache kumuangalia.
Wakati ambapo mnakuwa pamoja mnaongea, hakikisha kuwa macho yako yote yanamuangalia yeye kila wakati. Hii ni ishara ambayo itamuonyesha yeye kuwa una macho ambayo yanamzimia yeye pekeake. Mbinu hii itamfanya kwa urahisi kutaka kukutia machoni akuangalie kama bado tabia ya kumuangalia yeye uko nayo ama la. [Soma: Njia mbadala za kutongoza kwa kutumia macho]

#3 Usisahau kutumia lugha za kumsifu.
Ukweli usemwe. Watu wakiwa katika mahusiano kwa muda mrefu kuna vitu mbavyo wanavichukulia kama mzaha. Mfano katika mahusiano ya mwanamke na mwanamume, unapata mara nyingi wamezoeana kiasi cha kuwa wanajihisi uhusiano wao umeshikana kiasi cha kuwa wanasahau mambo madogo madogo kama vile kumsifu mpenzi wake, kumzawadi nk.
Hii ni njia wapo rahisi ambayo itakuwezesha wewe kuuteka moyo wa mwanamke ambaye ana boyfriend kwa haraka. Maneno ya kumsifu ambayo hajaambiwa kitambo yanaweza kumchanganya akili mwanamke yeyote na kumfanya kuingiwa na hisia mbili mbili. Niamini ukitumia mbinu hii utakuwa na nafasi kubwa ya kwako kufaulu kumpata mwanamke aina hii.

#4 Hakikisha umemuelewa ndani na nje.
Wengi wangeuliza itakuwaje kumfahamu mwanamke ndani na nje na tayari ana boyfriend? Kama ulikuwa hujui basi ni hivi, kulingana na utafiti, inasemekana kuwa akili ya mwanamke inafanya kazi tofauti kabisa na ya mwanamume. So usitilie shaka kabisa hapa. Pia hakikisha umesikiliza kila kitu ambacho atakwambia na utilie maanani yote atakayosema.

KUMBUKA: Wanawake hujiskia huyu kuongea yote ambayo yanatoka akilini mwao kwa mwanamume ambaye anamuamini na kumkubali. Hivyo ukiona umefikia level hii fahamu ya kuwa hauko mbali na kutimiza lengo lako kuu. Pia usisahau kutumia maneno ya uchezi ili kupunguza tenshen ambayo inaweza kuwa kati yenu.

ONYO: Usijaribu kumwambia moja kwa moja kuwa unamzimia na unataka kumpokonya kutoka kwa boyfriend wake kwa sababu hio haitafanya kazi kamwe. [Soma: Sababu nzuri za wewe kufanya mapenzi na rafiki yako]1 comment:

Jiunge na jamii yetu ya Facebook/App yetu ili uweze kutangamana na members na readers wetu wa Nesi Mapenzi ama ujitafutie mpenzi HAPA

Powered by Blogger.