'Zimwi Mtu' Ambaye Anawakabili Wanaume


Hello reader wa N.M blog,

Wakumbuka wakati ambapo tulikuwa watoto wadogo?

Kabla hujaenda kulala, ulikuwa ukifuata tabia ambayo ilikuwa lazima uitimize.

Wengine wetu walikuwa wakiangalia kwa makabati...

Wengine wetu walikuwa wakiangalia chini ya kitanda...

Wengine wetu walilala taa ya usiku ikiwa wazi...

Wengine wetu walikuwa wakiwauliza wazazi iwapo "zimwi mtu"(boogey man) atakuja kuwachukua usiku huo.

Tulikuwa na kipawa kikubwa cha kuwa na mawazo katika fikra zetu.

Fikra zetu zilikuwa za nguvu, nzito, na za ubunifu, ambazo zilitufanya tujenga dhana za majini ambayo hayakuwepo.


So huyo mtoto asiyekuwa na hatia alienda wapi? Well, huyo mtoto alikuwa mkubwa  na kusahau kuhusu "zimwi mtu" kwa sababu ilifika mahali akaanza kufikiria kudeti wanawake.

Na pindi tu alipoanza kudeti wanawake, huyu "zimwi mtu" aliruka na kuingia katika kichwa chake na kuanza kuishi katika akili yake.

Huu ndio ukweli mtupu.

Wanaume wengi mpaka sasa wanaishi na "zimwi mtu" katika vichwa vyao.

Hebu fikiria uoga unaokuwa nao wakati inapokuja kukutana na wanawake.

Fikia uoga unaokuwa nao wakati unapo approach mwanamke kwa mara ile ya kwanza kabisa, na fikra ambazo zinakuzuia wewe kuongea na mwanamke kama huyu.

Hizo fikra unazokuwa nazo wakati huo huwa ni huyo zimwi mtu. Huwa ni toleo la zimwi mtu wa ukubwani. Na kwa bahati mbaya ni kuwa watu wakubwa huwa na woga zaidi kuwaliko watoto wadogo.

Watoto wadogo huogopa vitu ambavyo havipo, na mpaka ile siku watakapoumizwa wakifanya jambo flani, wataendelea kulirudia jambo hilo mara kwa mara.

Wakati ulipokuwa mtoto mdogo ni mara ngapi ulikuwa ukicheza na kisu mpaka ile siku ulipogundua ya kuwa kujikata kidole chako haikuwa jambo zuri?

Lakini kama mtu mkubwa, ni mara ngapi ushawahi kuapproach mwanamke mrembo na akakukataa halafu ukakubali zimwi mtu aingie na kuitawala akili yako?

Umekubali zimwi mtu achukue kontrol katika akili yako.

Umejijengea zimwi mtu ambaye anakuwa na nguvu kuliko zimwi mtu yeyote yule ambaye ushawahi kumtengeneza katika fikra zako.

So tutafanyaje mpaka tumwondoe huyu jinamizi?

Tutafanyaje mpaka tuondoe huu uoga wa kuapproach wanawake?

Ni rahisi sana, tunaweza kukupatia motisha na uhakiki ambao unaweza kuurudia mara kwa mara mpaka ukuige. Lakini kiukweli ni kuwa zimwi mtu hajulikani wakati ambao anaweza kujitokeza.

Anaweza kuja wakati unaaproach mwanamke, wakati unapoongea,  wakati mko deti ama labda kabla ya kufanya mapenzi.

So itategemea na vile ambavyo utajipanga wewe kwa sababu hapa Nesi Mapenzi tumehakikisha ya kuwa tunautoa woga wowote ambao unaweza kukabiliwa wakati unapotangamana na wanawake. Soma chapisho la jinsi ya kutoa uoga kwa mwanamke plus usome machapisho mengine ambayo yameandikwa spesheli ya kukabiliana na tatizo la kuapproach.

No comments:

Jiunge na jamii yetu ya Facebook/App yetu ili uweze kutangamana na members na readers wetu wa Nesi Mapenzi ama ujitafutie mpenzi HAPA

Powered by Blogger.