Jinsi Ya Kumfanya Mwanamke Apagawe Kwako


Kumpagawisha mwanamke ni ile hali ya kumzuzua mwanamke kiasi cha kuwa unamfanya kukufikiria mara kwa mara, kukuota ndotoni na kuongea kukuhusu akiwa na marafiki zake.


Mbinu za kupangawisha mwanamke ni mbili, aidha unampagawisha bila kujitambua ama unampagawisha kwa kutumia maujanja. Uzuri ni kuwa wanaume wengi huwa na uwezo huu wa kuwapagawisha wanawake.

Lakini kuna baadhi ya wanaume huwa wanapata changamoto ikifikia hatua hii.

Kumpagawisha mwanamke si vigumu, ukifuata mbinu sahihi utafaulu.

Hizi ni baadhi ya mbinu za kutumia kumpagawisha mwanamke:

#1 Uwezo wako wa nishati.
Nishati inaweza kuwa na mkusanyiko wa vitu kadhaa, kama vile kuhisi kwa vipepeo ndani ya tumbo, kusuka, wasiwasi ama vitu tofauti kabisa. Kwa mtizamo wa moja kwa moja, nishati inahusiana na yote yale ambayo yanamfanya mwanamke kujiskia raha wakati anapokuona ama kutaka kuutumia muda wake mwingi akiwa na wewe.

Nishati inacheza nafasi kubwa katika mapenzi kama wataka kumtongoza mwanamke na ufaulu kwa urahisi. Ili kupeana nishati zaidi kila wakati unapokuwa na mwanamke, hakikisha kile kikuu unachohitaji kufanya ni kumchekesha, kumsapraiz, umguse kwa bahati mbaya mara kwa mara, kuwa mwenye michezo nk. Zote hizo zitamfanya kukufikiria wewe mara 24/7.

#2 Mbinu utakayoitumia kumsifu.
Kulingana na utafiti kutoka NBC unadai ya kwamba wanawake wengi hawajiskii huru kupewa ama kupokea sifa kutoka kwa wanaume. Lakini usikatwe na tamaa! Vile ambavyo utampongeza mwanamke inaweza kucheza pakubwa kufaulu kumpata mwanamke umpendae. Afterall ukimsifu kitofauti tofauti anaweza kukubali ama kukuona kama wewe ni mzaha kwake.

So kuhepa aibu kama hizi ndogo ndogo, unafaa umsifu mwanamke kwa jambo ambalo ni la kwake pekee, yaani kitu ambacho utamsifu nacho hakipatikani kwa mwingine. Mfano waweza kumakinika kwa kitu ambacho anafanya wakati flani na utumie ujuzi wako wa kiume kumsifia na jambo hilo. Mfano unaweza kumsifu kwa uwezo wake wa kuimba, kuchora, mtindo wake wa kutembea nk. [Soma: Mbinu ya kutongoza kwa wale wanaojifunza]

#3 Upambo wako.
Si lazima uwe mwanaume wa kuvutia ili umvutie mwanamke. Utafiti umebainisha kuwa wanawake hawavutiwi na urembo wa mwanaume, nywele zake wala ngozi yake. Mwanzo kuwa mrembo kama mwanaume kuna ubaya wake mwingi ikizingatiwa kuwa unaweza kuonekana kama pleya ambaye unapendwa na wanawake wengi.

Kile ambacho unachohitajika hapa ni uhakikishe kuwa unakuwa nadhifu kimwili na mavazi yako. Kufanya hivi kutakusaidia wewe kuonekana mtu timamu halikadhalika inakufanya wewe kujiamini wakati unapproach demu yeyote yule.

#4 Ujuzi wako wa kutangamana.

Lazima atleast uwe na ujuzi ambao utakusaidia wewe kuweza kutangamana na wengine. Kama mwanaume lazima uwe na ujuzi ambao utakusaidia wewe kutangamana na wengine kwa urahisi. Hii inamaanisha kuwa lazima uwe na ujuzi flani wa kuongea na wanawake ndipo utakapojua jinsi ya kumfanya apagawe na wewe. [Soma: Jinsi ya kuongea na mwanamke mara ya kwanza]

#5 Kiwango chako cha kujiamini.

Kitu cha mwisho ambacho ni muhimu kwako kuwa nacho ni kujiamini. Kujiamini ni njia moja wapo ya lazima uwe nayo ili uweze kuiteka hisia ya mwanamke yeyote yule.[Soma: Njia za kuwa na confidence kama mwanaume]

KUMBUKA: Vitu vyote tulivyoeleza hapo juu havitakuwa na manufaa yeyote iwapo hutaweza kujiamini kama mwanaume. Hivyo ni lazima kwako kuhakikisha kuwa mwanzo unajijenga kwa kuwa na confidence. Hii ni kuanzia kujitambua wewe mwenyewe bila kujishuku, kuongea bila woga wowote wala kutoingiwa na wasiwasi wakati wowote ukiwa karibu na mwanamke.



2 comments:

Jiunge na jamii yetu ya Facebook/App yetu ili uweze kutangamana na members na readers wetu wa Nesi Mapenzi ama ujitafutie mpenzi HAPA

Powered by Blogger.
##valentine ##valentine