Hatua 3 Za Kufuata Unapomtongoza Mwanamke


Kama unataka kumpata mwanamke unayemzimia bila tatizo lolote basi hakikisha unafuata kila kitu ambacho utasoma sahizi. Hii mbinu imeibwa kutoka kwa kitabu cha Jinsi Ya Kumtongoza Mwanamke: Kuanzia Hadharani Hadi Kitandani - ambacho nakipendekeza kwa yeyote yule ambaye yuko tayari kutumia maujanja ya mazungumzo kumnasa mwanamke yeyote.


Inaenda hivi...

Hatua #1: Angalia ishara.  Ufunguo wa kutongoza ni kuzijua na kuzivumbua ishara fiche kwa yale anayofanya na kutenda. Makinika na stori ambazo anaeleza, mambo ambayo anapenda kuongea na kila kitu ambacho kinaamsha hisia zake. Kumbuka hapa unamakinika na mwanamke na wala si wewe. Usijaribu kutoa maoni  yeyote bila kufikiria madhara yake. Unataka kumtongoza - na hautaki maoni yako yaonekane kama kipingamizi.

Hatua #2: Cheza na hisia zake.  Hapa jambo muhimu la kufahamu ni kuwa - kwa kuchagua mambo yafaayo kumwambia mwanamke, unaweza kubadilisha hisia zake hadi vile unavyotaka wewe. Huu uwezo wa 'kubadilisha' hisia za mwanamke ni jambo MUHIMU zaidi ya yote ikija katika maswala ya kumtongoza mwanamke.

Ingiza hisia nyingi iwezekanavyo katika mazungumzo yako kwake. Jibu stori zake na hisia zifaazo na utakuwa umejitenga mbali na wanaume wa kawaida ambao wanamuapproach.

Hatua #3: Mpe uhakikisho. Kila mwanamke (hata kama ni mrembo kiasi gani ama 'amekamilika' mbele ya macho yako) huwa wanakutojiamini ndani yao ambako kunahitajika kupewa uhakikisho kwa njia moja au nyingine. Hivyo hivyo, jambo muhimu la kuzingatia wakati unampa uhakikisho ni pale ambapo utakuwa mkweli wakati ambapo unampa huo uhakikisho.

Kumwambia kuwa ana macho mazuri hakutasaidia - hii ni kwa sababu maneno kama haya yashatumika mara kwa mara, na kila mwanaume anatumia maneno yayo hayo kama anataka kuingia ndani ya chupi ya mwanamke. Kumpongeza na kumpa uhakikisho kwa jambo ambalo hajiamini nalo kutamfanya akuthamini na kukuweka karibu na yeye zaidi. Na kama umefuata hatua hizi mbili za kwanza vizuri basi hautakosa kupata jambo ambalo litampendeza.

Huu uwezo wa kumtongoza mwanamke kwa kutumia maongezi ni advantage ya kikweli ambayo mwanaume anapaswa kuwa nayo. Ni jambo ambalo ni bora kuwa nalo kama unataka kuwa na nafasi nzuri kwa mwanamke yeyote.

5 comments:

  1. I love your blog.. very nice colors & theme. Did you make this website yourself or did you hire someone to do
    it for you? Plz respond as I'm looking to
    create my own blog and would like to find out where u got this from.

    cheers

    ReplyDelete
    Replies
    1. I created it. Contact me via my contact me page

      Delete
  2. Oh my goodness! Impressive article dude!

    Thanks, However I am experiencing difficulties with your RSS.
    I don't understand the reason why I can't join it. Is
    there anyone else getting the same RSS issues?
    Anyone who knows the solution can you kindly respond?
    Thanks!!

    ReplyDelete
  3. It's enormous that you are getting ideas from this article as
    well as from our discussion made at this time.

    ReplyDelete
  4. I know this site gives quality depending articles and
    additional information, is there any other website which presents these information in quality?

    ReplyDelete

Jiunge na jamii yetu ya Facebook/App yetu ili uweze kutangamana na members na readers wetu wa Nesi Mapenzi ama ujitafutie mpenzi HAPA

Powered by Blogger.
##valentine ##valentine