Jinsi Ya Kuuhepa Mtego Wa Kuwa Rafiki Na Mwanamke Unayempenda


Wakati unapotongoza mwanamke kuna mambo ambayo hupaswi kufuata ama kutumia. Kwa mfano ukiwa katika harakati ya kutongoza hupaswi kutumia mbinu ya kumfanya awe rafiki yako.


Kosa ambalo wanaume wengi hujuitia mbeleni ni pale wanapowafanya wanawake marafiki kisha wanaanza kuwatongoza. Mara nyingi mbinu hii itakutoa timing kiasi cha kuwa ile siku utafunguka kumwambia ukweli atakueleza kuwa amepata mpenzi ama anakuona wewe kama rafiki tu.

Hili kosa hupaswi kulifanya kamwe ndio maana leo tumekuja na mbinu ambayo unapaswa kuifuata ili uweze kumchumbia mwanamke bila kukuona kama rafiki yake.

#1 Kuwa rafiki yake lakini tofauti na marafiki zake wengine.

Msiongee vitu vya kijinga kwa masaa mengi ama mkae mnaongea kuhusu matatizo yake anayokumbana nayo maishani. Mnafaa muongee vitu kama sinema, sehemu anazotembea, vitu ambavyo anapanga kufanya wikendi nk. Ongea vitu ambavyo vinahusiana na kudate. Hapo utafanya kuwe na msisimko kati yenu.

#2 Jaribu kuongea mkiwa nyinyi wawili.
Kama yuko na marafiki zake wengine, unaweza kuongea na yeye ama ukaamua kutoongea kabisa manake hauwezi kumrushia matamu akiwa pamoja na kundi zima la marafiki.

Mkiwa wawili unaweza kujaribu kutumia maujanja ya kumsuka bila ya yeye kutambua halafu kama kumekuja mtu wa tatu fanya kujeuza stori haraka. Hii itamuacha yeye kujiuliza kama kweli ulikuwa unafanya mzaha ama uko serious.
Hii itampa fikra za kuwa wewe unapenda zaidi kuongea na yeye mkiwa pekeenu. Mwonyeshe dhahiri kuwa unapenda uwepo wake zaidi mkiwa wawili. Lakini chunga usithubutu kumwambia kuwa unampenda ama wataka kumtoa out.

#3 Msifu wakati ambapo inahitajika.
Kama amependeza usisahau kuchukua nafasi ya kumsifu. Pia unaweza kutumia ujanja wa kuchungulia kifua chake kisha kama amekuona ukimuangalia, fanya kutabasamu, mwombe msamaha halafu umwambie kuwa ulikuwa umeshindwa kujizuia. Jaribu kuongea kwa maneno ya ucheshi wa mapenzi na kutoa maoni ya mapenzi. Amini usiamini ataanza kukufikiria tofauti na utakuwa ukijinasua pole pole kutoka friend zone.[Soma: Jinsi ya kumfanya mwanamke apagawe kwako]

#4 Mshike na mchukulie kama ni girlfriend wako.
Lakini fanya na heshima. Unaweza kumshika mkono wakati mnavuka barabara na pia kumfungulia mlango. Mfanye ajihisi yeye kama malkia na ataanza kupenda ateshen yako. Akiwa na marafiki wengine usimwonyeshe dalili hizi. Mfanye aelewe kwamba hii inatokea kama mko wawili pekee.

#5 Mfanye ajihisi kuwa yeye ni spesho.
Mtuze kwa kumletea zawadi ndogo ndogo na binafsi mfano waweza kumletea ushanga, vipuli, vipodozi, nk lakini hakikisha kuwa umemwambia kuwa iwe siri kati yenu. Ukifanya iwe siri kati yenu utakuwa automatically unafungua mlango wa mapenzi na ataanza kukufikiria na mtizamo mwingine. Utakuwa mnajenga kemia kati yenu.

7. Muulize kama anataka kutoka out halafu ubadilishe stori fasta

Kama unaongea na yeye unaweza kumwambia kuwa unataka kumtoa lunch ama kwa mkahawa. Lakini kabla hajajibu fanya kumjeuzia topic nyingine ili abaki ajiuliza kama ulikuwa unafanya mizaha au la. Hivi itakuwa ikondoa tenshen ambayo itakuwa imejitokeza wakati wa kuuliza swali kama hilo.
[Soma: Dalili 7 za kuonyesha kuwa mwanamke anakupenda]

Hii ndio njia rahisi ya kutumia na mara kwa mara utaona kuwa amevutiwa na wewe. Baada ya muda flani unaweza kuchukua hatua ya kumuuliza kama angetoka date na wewe na hapo hawezi kukataa.


No comments:

Jiunge na jamii yetu ya Facebook/App yetu ili uweze kutangamana na members na readers wetu wa Nesi Mapenzi ama ujitafutie mpenzi HAPA

Powered by Blogger.