Kwa Nini Wanawake Wanapenda Wanaume Masharobaro


Wanawake kuchagua wanaume masharobaro ama kwa lugha ya kimombo badboys kuwaliko wanaume wa kawaida si jambo geni na hutokea mara kwa mara. Jambo hili tumeliona likitendeka aidha katika vyuo, vilabuni, sinema, maktabani ama sehemu yeyote ile. 


Wanaume masharobaro, kama wanaume wengine, wao pia wana maumbo ya kila aina, shepu na mvutio wa kijinsia. Kama wewe ni mwanaume wa kawaida ambaye humaliza wa mwisho ama ushawahi kupoteza mpenzi wako kwa sharobaro fulani, hapo chini kuna nadharia ambazo zitasaidia kueleza kwa nini  wanawake wanapenda sana kuvutiwa na wanaume masharobaro.

#1 Hamu ya kufuata.
Kufuata kitu ambacho unakipenda huwa kuna msisimko fulani mtu hupata. Lakini msisimko zaidi hutokea wakati ambapo mtu anajaribu kufuata mtu ambaye hataki kujulikana mienendo yake ya kimaisha, kufuatwa ama kueleweka kimaisha. Haya ndio maisha anayoishi mwanamume sharobaro.

Wanawake wanapenda sana wanaume ambao hawaeleweki kimaisha (yaani hawatambuliki) ama kutakwa kujua maisha yao. Na wewe kama mwanaume unataka kutumia huu udhaifu kwa manufaa yako, wakati mwingine unafaa kumfanya mwanamke abaki na maswali chungu nzima kutaka kukujua zaidi. Kama unampenda, jaribu kadri iwezavyo kutojaribu kumuonyesha.  Badala yake mpe pia yeye changamoto kwa kuweka ujanja wa kutoeleweka mara kwa mara. Hii ni njia moja murua ya kuhakikisha utaingia katika akili yake.

#2 Kutaka kuwajeuza tabia zao.
Kitu kingine ambacho wanawake huvutiwa kwa sharobaro ni kutaka nafasi ya kuwafunga fundo ama kuwajeuza tabia zao. Mwanamke kikawaida amezaliwa naturally na hisia za uzazi, yaani hutaka kujeuza mtu mwenye tabia ovyo kuwa na tabia nzuri. Hii huibua hisia halisi za uzazi ndio maana kama mwanaume unapaswa wakati mwingine kumsumbua mwanamke kihisia, kimawazo na kadhalika. Unafaa kuwa mpinzani lakini usiwe mhalifu. Unafaa kuwa hatari lakini usipitishe kiwango ambacho kitamwogopesha.

Kimtazamo, unafaa kumfanya mwanamke auonyeshe uke wake wote ili kujaribu kukubadilisha, mpe nafasi ajaribu kuubadilisha upande wako wa kiza na mwishowe kukufanya uwe mwanaume thabiti katika mchakato mzima.

#3 Uanaume uliothabiti.
Wanaume masharobaro (na si wale feki) karibu nyakati zote huwashinda wanaume wa kawaida kwa sababu ya mambo mawili makuu. Kwanza ni kuwa ni wanaume majasiri na pili wanaudhibiti uanaume wao kwa kuwa ngangari kimaisha. Kutoogopa kwao kwa jambo lolote ndiko kunawafanya wanawake kuvutiwa nao.

Wanawake wengi wanavutiwa na wanaume ambao ni hatari, ngangari na wenye nguvu kwa sababu si rahisi kuchezewa au kufanyiwa masihara. Ukisimama  kumtetea mwanamke kuhusu mahitaji yake na uovu, hii inamaana ya kuwa una uwezo wa kusimama kando yake na jambo lolote lile.  Kuweza kuonyesha level ya kuwa wewe ni mtu usiekuwa na woga wowote, unafaa kumwonyesha mwanamke wako kuwa una uwezo wa kuwa ngangari mahali popote pale ili mradi kumlinda yeye tu.

#4 Uoga wa kujitwika majukumu.
Wanaume masharobaro hupenda kuhepa majukumu yanayohusiana na mahusiano. Kwa wanawake ambao wana uoga huo huo wa kuwa na majukumu, masharobaro huwavutia sana na kuwaona kama hakuna wanaume wazuri kama hao. Wanawake aina hii hawatajitweka majukumu kwa kuwa hawana haja ya kujishughulisha na hisia za kimapenzi ambazo ni stress.

Pia ni habari njema kwa wanawake ambao wako tayari kwa uhusiano wa kimapenzi wa muda mfupi pekee. Lakini kama kawaida, mwisho wa siku lazima mwanaume sharobaro au mwanamke mtundu lazima kuna sehemu fulani ndani ya mawazo yake anatamani kuwa na mahusiano ya kudumu na pia kupendwa. Hivyo siri hapa ni kuipima miondoko yake na uangalie level yake ya kujitwika majukumu katika mapenzi halafu sasa uanze na hapo.


Mwisho ni kuwa upende usipende, wanaume masharobaro watakuwa na nafasi kubwa katika nyoyo za wanamke. Kuna kitu ndani yao ambacho kinawasababisha wanawake kuangua mwili mzima kihisia na kimapenzi kwao. Lakini hii haimaanishi kuwa lazima kila mwanaume ajeuke na kuwa sharobaro ili aweze kuwa na nafasi rahisi ya kutongoza mwanamke aliye kwa ndoto yake. Kile unachotakiwa kufanya ni kucheza mchezo mzima kiwastani. Daima unafaa kuwa vile ulivyo huku ukiingiza tabia flani za usharobaro hivi katika miondoko yako. Kama kuna kitu kizuri kati yenu wawili, basi pia kuna sehemu mbaya ambayo unaweza kuitumia ili ukajinufaisha nayo.



1 comment:

Jiunge na jamii yetu ya Facebook/App yetu ili uweze kutangamana na members na readers wetu wa Nesi Mapenzi ama ujitafutie mpenzi HAPA

Powered by Blogger.
##valentine ##valentine